Jumatatu , 18th Oct , 2021

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila, amewasihi vijana wa Kitanzania kujielekeza zaidi katika sekta ya kilimo yenye fursa kubwa ya kupata utajiri.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Kafulila

Amesema Tanzania ina kiwango cha chini cha umaskini dhidi ya wananchi wake, ikilinganishwa na mataifa mengineyo ya ukanda wa nchi za Afrika Mashariki, ambapo ameeleza kuwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa na nidhamu ya kazi ndiyo kielelezo cha mafanikio ya kiuchumi ulimwenguni kote.

RC Kafulila ameyasema hayo wakati wa kongamano lililoandaliwa na vijana wa Mkoa wa Simiyu, wanaosoma vyuo vikuu nchini, lililolenga kujadili masuala ya ajira, elimu na uchumi.