Ijumaa , 28th Oct , 2022

Halmashauri ya jiji la Tanga imewataka vijana kutumia fursa ya mikopo iliyopo ili waweze kujikwamua kiuchumi ili kujiepusha na vikundi vya kihalifu kama kile cha watoto wa ibilisi ambavyo vimekuwa vikiibia watu na kuwajeruhi maeneo mbalimbali ya jiji. 

Mkurugemzi wa Halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Spora Liana

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugemzi wa Halmashauri ya jiji la Tanga Dkt. Spora Liana, wakati wa kikao cha baraza la madiwani.

Mkurugenzi Liana amesema wanaendelea kuhamasisha vijana, akinamama na watu wenye ulemavu ili waweze kwenda kuchukua mikopo kwani wataalamu wamepangwa ili waweze kuwasaidia kupata mikopo ya asilimia 10 isiyokuwa na riba. 

Awali akizungumza katika kikao hicho Mstahiki Meya wa jiji hilo Abdulrahman Shiloo, amekazia kwenye suala la miradi na kueleza kuwa hivi sasa wana miradi ya madarasa 29 ambayo wamepata fedha kiasi cha shilingi milioni 580 kutoka Rais kwajili ya kuepuka uhaba wa madarasa kwenye mwaka wa masomo 2023.