Jumapili , 9th Oct , 2016

Mbunge wa Singida Magharibi Mheshimiwa Elibariki Kingu amewaasa viongozi wa siasa nchini kuacha tabia ya visingizio vya kushidwa kutekeleza majukumu yao kwa kisingizio cha kukosa pesa kutoka serikalini.

Mbunge wa Singida Magharibi Mheshimiwa Elibariki Kingu

Akizungumza na waaandishi wa habari Mbunge Elibariki amesema ni wakati sasa kwa viongozi wa siasa kuhakikisha wanashirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo kwakua wananchi wamewachagua viongozi hao kwa lengo la kusaidiana katika kuleta maendeleo ya eneo husika hasa kwa makundi maalum.