
na uhasama ili kuepusha nchi kuingia katika hali ya machafuko na mauaji yanayosababishwa na kupandikizwa kwa chuki.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Umoja wa Mataifa (UN) kupitia kwa Afisa Habari wake Bi. Usia Ledama wakati Tanzania ilipoungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya kimbari dhidi ya wayahudi wapatao milioni sita waliouwawa chini ya uongozi wa kinazi wa Adolph Hitler uliofanyika kati ya mwaka 1933 hadi 1945.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mauaji mengi ya kimbari yamekuwa yakisababishwa na watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii na hivyo endapo watu wenye ushawishi waliopo kwenye jamii kwa sasa wasipotumia nafasi zao ipasavyo kuimarisha upendo, amani na utulivu haswa kwa kuwaelimisha vijana jambo hilo lina hatari ya kutokea tena.