
Askofu Emaus Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Morovian
Askofu Mwamakula ameongeza kuwa vyombo vya habari vinatakiwa vitizamwe kwa jicho la upekee kwani ni mtumishi wa watu wote bila kuegemea upande wowote.
"Chombo cha habari tukione kwamba ni mtumishi wa wote katika nchi, hakipo pale kwa ajili ya kufurahisha kikundi fulani, chombo cha habari hakipo kwa ajili serikali, chama tawala, upinzani ama vyombo vya dini bali kwa jamii yote," amesema Askofu Mwamakula wa Kanisa la Uamsho la Morovian
Aidha Askofu Mwamakula ameongeza kuwa, "Vyombo vya habari vikiwa huru, maana yake vyama vya siasa vitaogopa kufanya mambo ya hovyo, chama tawala kitaogopa kufanya mambo ya hovyo,".
Askofu Mwamakula pia akasisitiza, "Katika ukombozi tunaoudai sasa hivi wa katiba mpya, utaendana pamoja na uhuru wa vyombo vya habari visiwekwe mfukoni na chama tawala, visiwekwe mfukoni na kikundi kinachoitwa CCM , visiwekwe mfukoni na vyama vya siasa,".