Alhamisi , 2nd Jun , 2016

Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania (TRA)imeanza kugawa mashine za EFDs Bure kwa wafanyabiashara wadogo na wakati ambapo mpaka sasa wameshatoa mashine kwa wafanyabiashara 5703 kwa Mkoa wa Dar es Salaam pekee.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi (TRA),Richard Kayombo,

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi (TRA),Richard Kayombo, amesema utekelezaji huo umeanza rasmi katika maeneo yote ya Jiji.

Bw. Kayombo amesema kuwa kuwagawa mashine hizo za Kieletroniki kwa wafanybaishara hao ni kuhakikisha kuwa kila mfanyabiashara analipa kodi stahiki na kwa wakati pindi anapotoa huduma.

Kayombo amesema kuwa licha ya kutoa mashine hizo bure lakini wameweka vigezo kwa kuweka kiwango maalumu cha Mauzo kwa mwaka ambapo nje ya hapo viwango atalazimika kulipia mashine hizo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi (TRA),Richard Kayombo,