Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Mary Mashingo, katika maonesho ya mifugo jamii ya ndege wafugwao, yanayolenga kutoa elimu kwa wafugaji waweze kuona, kutambua na kupata mbinu za namna bora ya ufugaji wa kisasa wenye tija na unaolenga kubadilisha maisha ya watanzania kiuchumi.
Daktari wa mifugo kutoka kampuni inayojishughulisha na utengenezaji wa vyakula vya mifugo na vifungashio Dkt. Christopher Israel Kileo amesema utengenezwaji wa chakula kwa teknolojia ya tambitambi unarahisishia mifugo kutumia na kukua kwa haraka pamoja na kupunguza magonjwa ya mifugo.