
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, ameagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa haraka kuwabaini watu waliohusika na hilo
Homera amesema mbali na moyo viungo vingine vilivyonyofolewa ni Ulimi na jicho la kulia huku tukio hilo likihusishwa na imani za kishirikina.
Mtoto wa marehemu wa Neema yuko hospitali ya Wazazi Meta chini ya uangalizi maalum wa madaktari akiendelea kupatiwa huduma za matibabu.