Ijumaa , 29th Oct , 2021

Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma tangu kuanzisha kwake utoaji wa huduma ya upandikizaji wa Figo, hadi sasa imefanikisha kupandikiza figo kwa wagonjwa 23 kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma, Dkt Alphonce Chandika

Kauli hiyo imetolewa hii leo Oktoba 29, 2021, na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Dkt Alphonce Chandika, alipotembelea ofisi za makampuni ya IPP Media Mikocheni Dar es Salaam, kwa lengo la kuona namna vinavyofanya kazi pamoja na kuvishukuru kwa kushirikiana na hospitali hiyo katika kufikisha habari za masuala ya afya kwa umma.

Kwa mujibu wa Dkt Chandika, Hospitali ya Benjamin Mkapa ya jijini Dodoma, ilianzishwa kwa lengo la kuweza kutoa huduma zote ambazo zilikuwa hazipatikani nchini na sasa ipo kwenye mpango wa kujenga jengo la utoaji wa huduma ya mionzi kwa kanda ya kati kwani huduma ya mionzi inapatikana Dar es Salaam peke yake.