
Pundamilia
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuhujumu uhai wa wanyama hao katika pori la Karabandea linalopakana na hifadhi za Taifa za Mkoamazi mkoani Kilimanjaro na Tsavo inayoambaamba Kusini Mashariki mwa Nchi jirani ya Kenya.
Mamlaka za serikali katika wilaya ya Mwanga zikiongozwa na mkuu wa wilaya Abdallah Mwaipaya ndizo zilizoanza harakati za kufuatia nyendo za watuhumiwa hao baada ya kupewa taarifa na wananchi.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Kamishina Msaidizi wa Polisi Simon Maigwa, amesema watu hao walitumia kuwauwa wanyamapori hao kwa kutumia bunduki na ambayo bado haijakamatwa .