Jumatatu , 7th Nov , 2022

Familia za watoto 70 nchini  Gambia waliofariki kutokana na majeraha ya figo , wanaodaiwa kuhusishwa na ulaji wa dawa za kikohozi zilizotengenezwa nchini India, zimekataa ofa ya fidia kutoka  serikali  ya nchi hiyo.

Baadhi ya wanafamilia

Wizara ya jinsia ilikuwa imetoa dola 20,000 sawa na zaidi ya shilingi 46,739,892 fedha za kitaznania   zitakazogawanywa miongoni mwa familia hizo.

Mwenyekiti wa familia zilizofikwa na misiba hiyo Ebrima Sanyang, amesema pesa hizo ni "matusi kwa waathiriwa".Alisema kukubali fedha hizo kunatafsirika kuwa hawapiganii haki.

Familia hizo zinataka shirika la serikali la kudhibiti dawa kuondoa madai yake ya awali kwamba watoto hao walikufa katika maji ya mafuriko na sio kutokana na dawa mbovu.