
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo SACP Lazaro Mambosasa, na kusema kuwa Jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa raia wema na kikosi kazi kilianza kufuatilia tukio hilo, ambapo pia amewaonya wakazi wa jijini humo kutojihusisha na vitendo vya uhalifu.
"Watu hao walikuwa ni tishio la usalama kwa majirani wa eneo hilo, na wakazi wa maeneo hayo walitoa dukuduku lao baada ya kusikia genge hilo la uhalifu limeuawa, natoa rai kwa wakazi wa Dar es salaam msivunje sheria za nchi", amesema Kamanda Mambosasa.
Tukio la kuuawa kwa majambazi hao limetokea Mtaa wa Kinyerezi kwenye nyumba moja ambayo walikuwa wakiishi majambazi hao.