Jumatatu , 9th Jan , 2023

Mamia ya wakulima wa Kijiji cha Ngabolo wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wameandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ambapo ni zaidi ya  Km 50 kutaka atatue mgogoro wa ardhi kati yao na hifadhi ya WMA ambao wanataka waondoke na wasifanye shughuli za kibinamu 

 

Wakizungumza kwa hisia kali baadhi ya wakulima hao wamedai kuwa mara kadhaa wamekuwa wakiahidiwa kukutana na Mkuu huyo wa Wilaya aje kutatua mgogoro huo bila mafanikio hivyo baada ya madhara kuanza kujitokea sasa wamelazimika kuandamana hadi ofisini kwake

Aidha maeneo hayo imedaiwa kuwa awali waliyapata kisheria na wengi wao waliweza kuyatumia kwa ajili ya mikopo kwenye taasisi za kifedha hivyo wameomba Serikali kuingilia kati ili madhara yasijitokeze zaidi

Akizungumza kwa njia ya simu Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga mbaye kwa sasa yuko likizo amesema, ili kutatua mgogoro huo kwa haraka wamejipanga Jan 10.2023 wataalamu kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo hayo watafika ili kubaini maeneo hayo