
Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe
Profesa Shemdoe ametoa kauli hiyo mkoani Shinyanga na kusema kwamba kwa nyakati tofauti amekuwa akipokea malalamiko yasiyoisha juu ya mkwamo huo wa baadhi ya barua za uhamisho kutokuwafikia watumishi waliopata uhamisho kwa wakati.
"Kumeibuka wimbi la baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa sehemu ya Masijala katika Ofisi za Mamlaka za Serikali za Mitaa kushindwa kutoa barua ambazo tayari zimesainiwa na Katibu Mkuu TAMISEMI na kutumwa kwenye Halmashauri, kwa ajili ya kuwapa wahusika lakini watu wachache kwa matakwa yao wamekuwa wakikwamisha barua kwenda kwa wahusika, hili halikubaliki na hii ni kwenda kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma,” ameonya Profesa Shemdoe.