Alhamisi , 20th Oct , 2022

Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda  Buriani, amewasainisha wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Tabora mikataba maalum ya usimamiaji wa shughuli zote za lishe  katika mkoa huo.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda  Buriani,

Akizungumza katika hafla fupi ya utiaji saini wa mikataba hiyo amesema, kufanya hivyo ni mkakati wa serikali nchini katika kukabiliana na tatizo la lishe duni kwa wananchi wake ikiwemo watoto na akinamama wajawazito.

Aidha amesema tatizo la udumavu wa watoto kwa Mkoa wa Tabora kutokana na lishe duni  lipo kwa 25% ambapo  katika hafla hiyo amewaagiza  wakuu wa wilaya  kuhakikisha wanakwenda kusimamia vyema shughuli zote za kuimarisha lishe kwa wananchi. 

Aidha amewaambia wakurugenzi watendaji wa halmashauri kuendelea kutenga fedha za lishe pamoja na kwenda kutumika kama ambavyo serikali imekusudia kuimarisha lishe  kwa wananchi wake na si kutumika  vinginevyo.