Jumatano , 15th Apr , 2020

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed, amesema kuwa wagonjwa wapya watano walioambukizwa Virusi vya Corona visiwani humo hawana historia ya kusafiri kwenda nje ya nchi siku za hivi karibuni.

Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed.

Tarifa hiyo imetolewa leo Aprili 15, 2020, wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa ugonjwa huo visiwani humo, ambapo leo ametoa taarifa ya wagonjwa wapya sita, ambaye mmoja ni raia wa Misri na kufanya visa vya wagonjwa wa Corona kufikia 18 na kifo kimoja.

"Wa kwanza ni mwanamme (37), mkaazi wa Fuoni, wa pili ni mwanamme (45) mkazi wa Pangawe, wa tatu ni mwanamme (63) aliyefariki Aprili 11 na kuzikwa, wa nne ni mwanamme (60) mkazi wa Migombani, wa tano ni mwanamke (48) mkazi wa Migombani, wa sita ni mwanamme Raia wa Egypt (33) ameingia nchini akitokea Dubai" imeeleza taarifa hiyo.