Ijumaa , 5th Sep , 2025

Maporomoko hayo ya ardhi yalipiga Milima ya Marrah, eneo la Urithi wa Dunia linalojulikana kwa hali ya hewa yake ya baridi na mvua, ambayo sasa imevunjwa.

Miili 375 imepatikana na kuzikwa kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyolikumba eneo la Darfur nchini Sudan huku vuguvugu la Ukombozi wa Sudan likionya kwamba idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka hadi 1,000.

Umoja wa Mataifa unasema ukubwa kamili wa maafa bado haujafahamika. Eneo hilo liko mbali, karibu haliwezi kufikiwa, na hivyo kuchochea hofu kwamba jumuiya nzima imetoweka.

Sudan ambayo tayari inasumbuliwa na vita vya kikatili vya miaka miwili kati ya Mkuu wa jeshi Abdel Al Burhan dhidi ya kamanda Mohamed Hamdan Dagalo   hivi sasa inakabiliwa na tabu kubwa zaidi.

Maporomoko hayo ya ardhi yalipiga Milima ya Marrah, eneo la Urithi wa Dunia linalojulikana kwa hali ya hewa yake ya baridi na mvua, ambayo sasa imevunjwa.

Sehemu kubwa ya eneo lililokumbwa na mzozo la Darfur limekuwa haliwezekani kufikiwa na Umoja wa Mataifa na mashirika ya misaada, kutokana na vikwazo na mapigano kati ya jeshi na RSF.