Rais Magufuli akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo
Katika ukaguzi wa Mei, Rais Magufuli alibaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.
Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.
Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili walitoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.
"Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua" amesisitiza Dkt. Magufuli.