
Ng'ombe
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 24,2022 wakati mtoto huyo akiwa machungani na ndipo alipokutana na watu hao kwa lengo la kuiba Ng'ombe wanne aliokuwa akiwachunga mtoto huyo.
Hata hivyo,DC Jamila amesema ng'ombe hao wamepatikana na wahusika wote wamekamatwa.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbugani Boniface Senegali, amesema kilio kikubwa cha wananchi kwa serikali ni kuwajengea kituo cha Polisi kwani wanadai usalama kijijini hapo umekuwa mdogo kutokana na vitisho na vitendo vya wizi kushamiri.