Jumamosi , 17th Sep , 2022

Wanafunzi waliopata ujauzito na kusitisha masomo yao ya msingi au sekondani Mkoani Lindi, wametakiwa kurudi shuleni mapema ili waweze kuendelea na masomo jambo litakalowasaidia kuweza kutimiza ndoto zao.

Picha ya mwanafunzi mwenye ujauzito

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga katika kilele cha siku ya Elimu ya watu wazima nchini,  ambapo Mkoani Lindi kilele hicho kimefanyika katika Halmashauri ya Mtama. 

Kwa upande wake Mariam Yusuph ambaye ni binti aliyerudi masomoni baada ya kupata ujauzito, anawasihi wengine kurudi shule kutimiza ndoto zao.