Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla
Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 24, 2022, mara baada ya kupokea taarifa ya tume iliyoundwa ili kuchunguza ni nini hasa chanzo cha moto huo uliotokea usiku wa kuamkia Januari 16 mwaka huu na kupelekea karibu asilimia 98 ya soko la Karume kuteketea kwa moto.
"Sasa zile hisia za nani kachoma nini, mmeona wenyewe, tumeelezwa na mmemsikia Jose amejitoa mhanga ameeleza kwamba tusipoteze muda aliyechoma soko ninamjua, ninaamini jeshi la polisi litachukua hatua stahiki kwa sababu watu hao wanajulikana," amesema RC Makalla





