Ijumaa , 31st Jul , 2015

Wananachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa wamekumbushwa kujitokeza kwenye zoezi la kuwapigia kura ya maoni wagombea wa ubunge na udiwani ili kpata viongozi bora.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akiongea na Wananchi

Katibu wa CCM wilayani Iringa Vijijini Bw. Dodo Sambu amesema zoezi la kupiga kura za maoni litafanyika Agosti Mosi mwaka huu kwa ajili ya kumpata mgombea mmoja kwa nafasi hizo.

Bw. Sambu amesema kura za maoni zitapigwa katika vituo vya matawi ya chama cha CCM kwa ngazi ya kata na litafanyika kwa siku moja na wanachama watatumia kadi zao.

Naye Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Iringa Bw. Ally Nyawenga amewataka vijana kujitokeza katika zoezi hilo.

Hata hivyo, Bw. Nyawenga amewataka vijana kuwa makini na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaowatumia kwa manufaa yao binafsi.