Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wanafunzi mbaroni kwa kumdhalilisha mwenzao

Jumapili , 29th Jan , 2023

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema kuwa limefanikiwa kuwakamata wanafunzi wawili wa chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanafunzi wa chuo hicho kwa njia ya mtandao na wanafunzi wenzake

 

Akitoa taarifa hiyo leo Januari 29,2023 Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amewataja waliokamtwa kuwa ni Efron Isaya (32) na Cosmas Robert (26) wote wakiwa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru

Kamanda Masejo amesema kuwa Januari 21 mwaka huu muda wa saa 11:00 jioni huko katika Chuo cha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (CDTI)  kilichopo wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha kuliripotiwa tukio la unyanyasaji wa kijinsia mwanafunzi wa chuo hicho  (jina tumelihifadhiwa) kwa njia ya mtandao na wanafunzi wenzake.

ACP Masejo amesema baada ya kupata taarifa hiyo jeshi hilo lilianza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na kufanikiwa kuwakamata wanafunzi hao wawili. 

Masejo amesema bado Jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Sambamba na hilo Polisi mkoani humo wametoa onyo kwa watu wachache ambao wana matumizi mabaya ya mitandao inayodhalilisha utu na heshima ya jamii yetu ya Kitanzania ambapo amewataka kuacha mara moja tabia hiyo kwani Jeshi hilo litawachukuliwa hatua kali za kisheria
 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya