Jumanne , 15th Feb , 2022

Wanafunzi katika shule ya msingi Kasaba kata ya Kidahwe halmashauri ya wilaya ya Kigoma wako hatarini kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia msituni kufuatia shule hiyo kutokuwa na huduma ya vyoo tangu mwaka 2020 baada ya kutitia.

Vyoo vya shule ya msingi Kasaba vilivyotitia na kulia ni baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo

Wakielezea adha hiyo wanafunzi wamesema kwanza hawana maji wala vyoo kwani vilititia na shule ilichimba mashimo machache ya muda ili yawasitiri ambayo hata hivyo asilimia kubwa hawayatumii kwa kuhofia usalama wake kwani yamekuwa yakibomoka mara kwa mara.

Aidha, wanafunzi hao wameongeza kuwa shule hiyo pia inakabiliwa na upungufu wa madarasa ambayo hulazimisha wanafunzi kurundikana huku kukiwa na vyumba vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi ambavyo hadi sasa havijakamilishwa.