
Martina Kabisama, mratibu wa SAHRINGON Tanzania.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC na muungano wa asasi za kiraia kwa nchi za kusini mwa Afrika SAHRINGON tawi la Tanzania ambayo inakituhumu CCM kuwa kilihusika na unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwadhalilisha wabunge wanawake kama anavyoeleza mkurugenzi mkuu wa SAHRINGON Tanzania Bi. Martina Kabisama.
Wakati CCM wakituhumiwa kwa udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia; Chadema wao wanatuhumiwa kwa kutoa kauli zinazoashiria vitisho na uvunjifu wa amani ambapo kwa mujibu wa Bi. Kabisama, baadhi ya kauli zilizotolewa na chama huenda ziliwatisha wananchi na pengine kuathiri zoezi la upigaji kura.