
Putin ameyasema hayo alipokutana viongozi wa wabunge mjini Moscow ili kujadiliana kuhusu idadi ya wanajeshi wastaafu watakaoajiriwa tena.
Hivi karibuni, wataalam wa masuala ya kijeshi walikadiria kuwa idadi ya wanajeshi wa Urusi ikiwa ni pamoja na wale waliotumwa nchini Ukraine, hawazidi wanajeshi milioni 1.3 huku wanajeshi wa Ukraine wakikadiriwa kufikia 900,000.
Hayo yakiarifiwa, Moscow na Kiev zimeendelea kushambuliana huku rais wa Marekani Donald Trump akitaja kufadhaishwa na Putin kwa sababu hajakubali kukomesha vita nchini Ukraine na kwamba Marekani itasaidia kuhakikisha amani baada ya vita hivyo kumalizika.
Katika hatua nyingine Urusi na Ukraine zimebadilishana miili ya wanajeshi zaidi ya 1,000 waliouawa katika vita, mamlaka ya Ukraine imesema kulingana na Aljazeera. Kyiv inabainisha kwamba kubadilishana huku kwa miili ya wanajeshi na Urusi kunakuja wakati Ukraine inadai kusonga mbele mashariki mwa nchi.
dadi kubwa ya miili hiyo ilipokelewa kutoka Urusi na Ukraine, huku miili ya wanajeshi 24 wa Urusi ikikabidhiwa na Ukraine.
Ubadilishanaji wa miili ulisimamiwa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, kulingana na mradi wa Ukraine "Nataka Kupata".
Makumi ya maelfu ya wanajeshi wameuawa kwa pande zote mbili tangu uvamizi wa Urusi. Walakini, Kyiv wala Moscow hawatangazi data mara kwa mara kuhusu hasara zao wenyewe.