
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema
Elimu hiyo ni pamoja na kuhakikisha suala la usafi wa mazingira linapewa kipaumbele na kuwatahadharisha wananchi kuacha tabia ya kushikana mikono na kusalimiana kwa kukumbatiana.
Akizungumza kwenye kikao cha kamati ya huduma za afya ya msngi Mkoa wa Shinyanga juu ya kupambana na ugonjwa wa Ebola,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema,amewataka wataalam wa afya kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii ili ipate uelewa na kuchukuwa tahadhari ya kukabiliana nao licha ya kuwa bado haujaingia nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt Faustine Mlyitu na mratibu wa magonjwa ya kuambukiza Mkoa wa Shinyanga Mussa Makungu wakaeleza hatua walizochukuwa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.