Jumanne , 7th Jul , 2020

Polisi jijini Nairobi mchana huu wa Julai 7, 2020, wamelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika mitaa mbalimbali ya jiji la Nairobi.

Moja ya mitaa ambayo ilikuwa na maandamano

Mwandishi wa East Africa Television jijini Nairobi Dennis Chisaka ameripoti kuwa wakazi hao wa Nairobi wameamua kuingia barabarani wakipinga mauaji holela ya raia.

Chisaka amefafanua kuwa waandamanaji wanadai mauaji hayo yanafanywa na polisi.

Hata hivyo hali inazidi kuwa shwari baada ya polisi kudhibiti.
 

Tazama Video hapo chini