Jumamosi , 5th Nov , 2022

Wananchi wa Wilaya ya Kalambo wametakiwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha miradi ya maendeleo ikiwemo zahanati na vituo vya afya vinakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akishiriki kazi za ujenzi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga ametoa wito huo Novemba 04,2022 wakati alipofanya ziara ya kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa Oktoba 20 mwaka huu kwa uongozi wa Wilaya ya Kalambo kuhakisha miradi ya afya ya zamani inatengewa fedha na kukamilishwa.

Sendiga ameongeza kwa kusema ziara zake kwenye halmashauri zinaendelea ili kuhakikisha Rukwa inaondokana na uwepo wa miradi viporo hususani kwenye sekta ya afya.

“Nawataka watendaji wote wa serikali kwenye mkoa huu wawajibike ili kuleta matokeo chanya kwa kutatua changamoto za miradi ya maendeleo. Nitahakikisha ninafika maeneo yote kuwatatulia kero wananchi na kuwa hakuna changamoto katika utendaji tutashindwa kuitatua” Amesema Mkuu wa Mkoa Rukwa, Queen Sendiga.