Jumatano , 10th Dec , 2014

Wananchi wilayani Ruangwa mkoani Lindi wameitaka serikali kuchukua hatua juu ya mwekezaji wa Kampuni ya Utafiti wa Madini, mkoani humo baada ya kufanya utafiti huo miaka sita bila kutoa ripoti yoyote wala kuchangia miradi yoyote ya maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mh. Aggnes Hokororo.

Wakizungumza wananchi hao wamesema kwa miaka sita wameshudia maroli yakiondoka na udongo katika eneo hilo na hakuna taarifa yoyote juu ya mafaniko ya utafiti huo zaidi ya kuona wanaibiwa rasilimali zao bila faida yoyote.

Akizungumzia hali hiyo mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Rubeni Mfini amekiri kuwepo kwa kampuni hiyo na kusema kuwa inakuwa vigumu kutatua mgogoro huo kutokana na kukosekana ofisi ya madini katika wilaya hiyo.

Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa kilio cha wananchi hao walishakipeleka kwa mkuu wa wilaya hiyo Mh. Agness Hokororo, ambaye tayari ameshamwandikia Katibu Mkuu ambaye amesema kuwa Waziri wa Nishati na Madini atatembelea eneo hilo ili kutatua mgogoro huo.