
Pichani wananchi wa mtaa wa chakula Bora wakivunja kingo za mifereji.
Wakizungumza na Kurasa wananchi hao wamesema wamefikia uamuzi huo kutokana na kutoa taarifa tangu awali juu ya mifereji hiyo kutowekwa njia za kupitisha maji kutoka majumbani
“Haya tuliyafahamu siku nyingi na tulitoa taarifa mpaka kwa uongozi wa mtaa na hata mkandarasi tulimweleza lakini hatukusikilizwa” amesema Rehema mkazi wa Chakula Bora
Wakazi hao wameiomba serikali kuwasaidia ili tatizo hilo lisijirudie kila mara mvua inaponyesha.