
Kwa mujibu wa watafiti afya mbaya inaweza kuvuruga usingizi - lakini usingizi duni pia unaweza kuwa hatari zaidi kwa afya.
Kuna ushahidi usingizi husaidia kurejesha, kupumzika na kufufua mwili na akili , Utafiti wa uliofanywa na PLoS Medicine uliangazia afya na usingizi wa watumishi wa umma nchini Uingereza.
Washiriki wote wapatao 8,000 waliulizwa, Una saa ngapi za usingizi kwa wastani wa wiki?"
Wengine pia walivaa kifaa maalum cha kunasa muda ambao mtu amelala usingizi , kifaa ambacho kilivaliwa kama saa ya mkono.
Washiriki hao walichunguzwa magojwa sugu, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa kisukari, saratani na ugonjwa wa moyo, zaidi ya miongo miwili ya ufuatiliaj.
Wale waliolala saa tano au chini ya umri wa miaka 50 walikuwa na hatari kubwa ya kupata maradhi mengi kwa asilimia 30 kuliko wale waliolala saa saba. Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha London na Chuo Kikuu cha Paris Cité, kwa ujumla wanapendekeza kuhusu saa saba au nane za mtu kupata usingizi wa kutosha.