
Chapati
Akizungumza na kituo cha Radio cha Uganda Network, Msemaji wa Polisi wa mkoa wa Karamoja, Michael Longole, amesema kwamba hatua hiyo imekuja baada ya kubaini kwamba watu wengine hununua chapati zaidi ya tano na kuwapelekea wezi waliojificha vichakani baada ya kukimbia makazi yao.
Aidha, Longole alisisitiza kwamba huenda kwa kufanya hivyo kutawalazimu wezi hao kutoka mafichoni na kusalimisha silaha walizonazo.