Jumatatu , 30th Jan , 2023

Baraza la Taifa la Uhifadhi Mazingira (NEMC), limezitaka taasisi za utafiti nchini kufanya utafiti kufuatia kuwepo kwa tafiti zisizo rasmi zinazoeleza kwamba, ukataji miti hovyo unafanya hewa ya ukaa kuongezeka na kusababisha watu wanapopanda kwenye daladala kuanza kusinzia.

Daladala

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi la upandaji miti Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Hamadi Kisiwa amesema watu hao sio kwamba wanasinzia wana usingizi lakini  ni Ile hewa wanayovuta imekuwa na Carbon dioxide nyingi tofauti na watu wanapopanda magari yaliyofungwa vioo.

Kuhusu umuhimu wa kupanda miti kwenye jamii Meneja huyo amehimiza kuwepo kwa utaratibu wa mara kwa mara wa kupanda miti hasa kwenye mashuke ili kuwajengea uwezo wanafunzi wa utunzaji wa mazingira.