Alhamisi , 15th Dec , 2016

Idadi ya watu wanaotumia huduma za kifedha kupitia simu za mkononi imeongezeka kutoka asilimia 61 mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 80 mwaka 2016.

Takwimu hizo zimezotolewa na shirika la utafiti la TWAWEZA ambapo asilimia 79 ya watumiaji wa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu wanasema wanaridhishwa na huduma zinazotolewa huku mtumiaji mmoja tu kati ya kumi sawa na asilimia 10 amesema kutoridhishwa na huduma hizo kutokana na wao kutoridhishwa na huduma na gharama kubwa za huduma za kifedha kwenye simu za mikononi na huduma za kibenki.

Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania idadi ya watanzania waliokuwa wamefikiwa na huduma na kifedha kupitia simu za mkononi ilikuwa asilimia 50 mwaka 2014.

Kutokana na utafiti huo, shirika hilo limesema ni wajibu wa makampuni ya mitandao ya simu za mikononi, benki na taasisi nyingine za kifedha kufanya kazi kwa pamoja na kutoa huduma zitakazowasaidia wale ambao hawajafikiwa na huduma hizi muhimu.”