Wanaotumia watu wenye ulemavu kujinufaisha waonywa

Jumatano , 16th Sep , 2020

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume, amesema kuwa kumeibuka wimbi la watu wanaotumia walemavu kujipatia kipato kwa kuwa ajiri vijana wanaowatembeza walemavu katika maeneo mbalimbali Jijini humu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Rashid Mfaume

Dkt. Mfaume amesema hayo leo, katika kikao kazi cha maafisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Dar es Salaam, ambapo amewataka wanaofanya hivyo kuacha mara moja na wao kama mkoa wanafuatilia wahalifu hao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng’wilabuzu Ndwata Ludigija, amesema kuwa zaidi ya kaya 10000 jijini Dar es Salaam zimeanza kunufaika na mfuko wa afya wa jamii ikiwa ni mpango wa kuhakikisha huduma za afya zinawafikia watanzania wote kwa usawa bila kujali vipato vyao.

Wadau walioshiriki katika kikao kazi hicho, wamesema kuwa mikopo kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu itolewe mapema ili kutekeleza miradi kwa wakati.