
Mifuko ya saruji
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, wakati akizungumza na wafanyabiashara wa mkoa huo juu ya hali ya kupanda kwa bei ya saruji bila sababu za msingi, ambapo amesema serikali imefanya uchunguzi na kubaini kuwa, manispaa ya Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kuuza saruji bei ya juu, ukilinganisha na maeneo mengine hapa nchini jambo ambalo haliwezi kukubalika.
"Manispaa ya MOrogoro ndiyo kwanza nchi nzima kupandisha bei ya saruji, niwahakikishie hatukubaliani kabisa kitakachotokea nitakaponyanyuka ni lazima tukue hatua za kisheria na hatua ya kisheria ni kesi ya uhujumu uchumi", amesema RC Sanare.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara mkoani humo, wameiomba serikali kuzuia usafirishwaji wa saruji nje ya nchi ili ipatikane kirahisi, ikiwa ni katika kukabiliana na mfumuko wa bei, ambapo walieleza kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea kuongezeka kwa gharama ni pamoja na uwepo wa foleni kubwa viwandani katika upakiaji wa mizigo na kusababisha magari kutumia muda mrefu safarini.