
Hivi karibuni #EATV iliripoti habari ya kusimama kwa ujenzi kwa kituo hicho tangu mwaka 2017 licha ya serikali kutoa fedha zaidi ya Milioni 600 kwa ajili ya ujenzi
Agizo hilo amelitoa wakati alipotembelea kituo hicho cha Afya na kukuta majengo yamesimama ujenzi wake tangu mwaka 2017 na baadhi ya vifaa vya ujenzi vikiwa vimenunuliwa na kuwekwa stoo bila ya kufanyiwa matumizi.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Dk.Festo John ametoa mwezi mmoja na siku 14 kwa Halmashauri ya wilaya ya Tarime kukamilisha ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Bukira baada ya serikaIi kuu kutoa kiasi cha shilingi Milioni 470
Aidha Naibu Waziri ameagiza kufanyika kwa uchunguzi juu ya matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milion 470 zilizoletwa kwa ajili ya ujenzi mpya ya Sekondari ya Gicheri Halmashauri ya mji wa Tarime