Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Warundi mrudi nchini kwenu - Rais Magufuli

Alhamisi , 20th Jul , 2017

Rais John Magufuli amewataka wanachi wenye asili ya urundi waliopo nchini Tanzania wafanye wawezavyo kwa hiari yao warudi kwao wakaijenge nchi wasisingizie kuna vita kwa kuwa Rais wao Pierre Nkurunziza ameshawahakikishia kuwa kuna amani ya kutosha.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akihutubia wakazi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika viwanja vya Posta baada ya kupokea ugeni kutoka nchini Burundi wa rais huyo pamoja na baraza lake la mawaziri mchana wa leo uliyokuja kwa mazungumzo ya kiuchumi.

"Ndugu zangu warundi mmesikia taarifa iliyotolewa na Rais Nkurunziza anawaomba mrudi kwenye nchi yenu, mkajenge nchi yenu, mkajitafutie maisha. Ni kama wanaotoka Afrika kwenda Itali lakini kuna wakimbizi wamezoea kukimbia tu, sasa kwa sababu Rais ameshawaambia murudi nyumbani sasa mchukue hatua za kurudi nyumbani kwa hiyari wala sisi hatuwafukuzi. Ninafahamu wapo baadhi ya watu ambao hufanya biashara na wakimbizi kwa sababu ndipo wanaotoa vyakula, wanaomba misaada kule nje ya kusema kuna wakimbizi sana na saa zingine wanaelezea hali ambayo haipo", amesema Rais Magufuli. 

Pamoja na hayo Rais Magufuli ameendelea kwa kusema "nimesikia wakimbizi wengine wameahidiwa kwamba mtakuwa mnapewa  elfu kumi kumi wabaki sasa nasema wakawapeni hizo hela mkiwa Burundi, nataka tuelezane ukweli kwasababu tunawajibu wa kulinda amani katika nchi zetu na Mhe. Rais ameshazungumza hapa lakini nchini Tanzania tumekuwa na uzalendo mzuri kwamba wakimbizi wanapokuja muda mwingine tunawapa uraia. Sasa kama wapo watu wanakimbia kule kwa sababu waje tuwape uraia waziri wa mambo ya ndani simamisha zoezi la kuwapa uraia wanaokuja huko".

Rais Magufuli akiwa na wageni wake kwenye uwanja wa Posta.

Aidha, Rais Magufuli ameunga mkono ombi la Rais wa Burundi aliyowataka wananchi wake warundi kwao wakaijege kwa pamoja nchi hiyo kwa kuwa hakuna shida ya aina yoyote katika kipindi hiki.

"Na mimi niwaombe nitoe wito kwa ndugu zangu wa Burundi kwa hiyari yao mimi siwafukuzi ila kwa hiari yao warudi nyumbani na niwapongeze wale laki moja na hamsini elfu waliorudi kwa hiari yao pia niyaombe Mashirika yanayoshughulikia wakimbizi waache kuwahubiri wakimbizi kwamba Burundi kuna matatizo, waanze kuhubiri amani ya kweli kwamba wanao uwezo hawa wakimbizi kwenda Burundi", amesisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amemthibitishia Rais Nkurunziza kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa majirani zake wote waliopo ndani ya Afrika Mashariki ndani ya SADC pamoja na nchi ya Burundi.

HABARI ZAIDI

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil

Baadhi ya Wabunge Wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi

Serikali yashauriwa kuwa bunifu sekta ya usafiri

Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda

Watatu wanusurika kifo, scania ikimgonga bodaboda

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi (kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi (kushoto) wakimpatia vifaa kinga mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa madereva bodaboda wa jiji la Arusha.

Bodaboda 200 Jijini Arusha wanolewa na kufundwa

Rajab Abrahaman Abdalah, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga

CCM Tanga yaijibu CHADEMA kuhusu huduma za kijamii

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama

Wazazi simamieni maadili kwa watoto 

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani