Jumanne , 21st Dec , 2021

Shule ya Sekondari Nyachiluluma iliyopo mkoani Geita, inakabiliwa na ukosefu wa mashine ya kuchapishia hali inayopelekea wanapohitaji kuchapisha mitihani au nyaraka za serikali kusafiri zaidi ya kilomita 60 kufuata huduma hiyo.

Mashine ya kuchapishia (Printer)

Hali hiyo imepelea mbunge wa Viti maalum mkoa wa Geita Rose Busiga, kutoa msaada wa kompyuta tano na mashine moja ya kuchapa mitihani ili kupunguza changamoto hiyo.

Akizungumza shuleni hapo mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo  mkuu wa shule hiyo Guido Kyalyenda anasema kwa umbali waliokuwa wanasafiri ulikuwa unapunguza usalama wa mitihani waliyokuwa wanatunga kwa wanafunzi.

Tazama video hapa chini