Alhamisi , 29th Sep , 2022

Umoja wa Posta Afrika (PAPU), umesema hautamfumbia macho mtu yeyote atakayejaribu kutumia Posta kama njia ya kusafirisha mihadarati kwani haitasita kumchukulia hatua kali dhidi yake.

Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo

Hayo yamebainishwa na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo, jijini Arusha, wakati wa mafunzo ya usalama kwa wakuu wa Idara za Usalama za Posta Afrika yanayofanyika jijini Arusha yakilenga  kuwajengea uwezo na ubora katika utoaji huduma kwa njia ya teknolojia.

Matarajio ya mafunzo hayo ni kuona wataalamu wa  Shirika la Posta Tanzania na Afrika wanaongezeka na kuendana na mabadiliko ya teknojolia ili kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia usalama wa wateja.

Baada ya mafunzo haya siku tatu kutamatika na kufaulu yataiwezesha Tanzania kupata cheti cha uthibitisho cha kimatifa  kuwa ni salama katika kutoa huduma za Posta.