
Wakati zoezi la uokoaji likiendelea imebainika kuwa watu 30 walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakihusika na ujenzi wa jengo la ghorofa mbili lililoporomoka Jana jioni katika Kijiji cha Sembeti wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro Simoni maigwa amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mkuu wa wilaya ya moshi abasi kayanda amezunguzia tukio hilo na kuwataka wananchi mkoani hapa kufuata sharia na kanuni wakati wa kufanya ujenzi ikiwa ni pamoja na upimwaji wa eneo husika kwani sio kila eneo linastahili kujengwa ghorofa