Ndege iliyobeba watanzania
Idadi hiyo inahusisha wanafunzi 150, watumishi wa Ubalozi 28 na diaspora 22.
Wamo pia raia wa nchi za Marekani, Uingereza, Kenya, Uganda, Sierra Leone, Malawi, Zambia na Msumbiji ambao wote kwa pamoja walisafirishwa kwa mabasi kwa siku mbili kutoka Khartoum, Al Qadarif, Metema hadi Gondar zaidi ya kilometa 900.
Safari yao ilinza kwa mabasi majira ya saa 7.30 mchana Aprili 24, 2023 kuelekea Mji wa Al Qadarif ambao upo takribani kilomita 420 kutoka Khartoum.
Ambapo awali walitembea kwa miguu kutoka kwenye makazi yao kwenda meeting point - International University of Africa (IUA), Khartoum na kwenda Al Qadarif hadi Metema mpakani Ethiopia na pia kusafiri kwa ndege kutoka Gondar kwenda Bole Addis Ababa.
Akizungumza bungeni Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt Stergomena Tax, alisema kwamba serikali inafanya jitihada za kuwaondoa raia wake walioko nchini Sudan, baada ya nchi hiyo kukumbwa na machafuko ya mapigano ya wao kwa wao.