Naibu Mkurugenzi wa mafunzo kutoka chuo cha Diplomasia nchini Dkt.Kitojo Watengere amesema Tanzania imekua ikisuasua kutoka hapa ilipo kwa sasa kwasababu baadhi ya viongozi wamekosa uweledi katika utendaji wa kazi zao na kuelekeza nguvu kubwa kwenye maswala ya ufisadi.
Dkt.Kitojo ameyasema hayo jijini Dar es salaam kwenye mahojiano maalumu na East Africa Radio nakuongeza kuwa pesa zinazopangwa kwaajili ya maendeleo ya nchi ni razima sasa serikali na wadau wa maendeleo kuhakikisha zinatumike katika kuleta maendeleo ya nchi hasa kupeleka huduma muhimu kwa wananchi.
Amesema kulingana na mapungufu yaliyopo kwa sasa wananchi na viongozi wanawajibu wakuhakikisha wanapambana na mafisadi bila uwoga na viongozi kuhakikisha pesa zinazopatikana ni razima ziguse maisha ya wananchi bila ubaguzi na kupambana na mafisadi bila kuchoka.
Amesema kuhusu eneo la mapato ya taifa ni razima sasa kuangalia namna yakubadilisha aina ya kuingia mikataba mbalimbali ya kimataita na kitaifa ambayo imekua ikikwamisha Serikali kupata mapato yake yaliyokusudiwa ambayo yangeweza kusaidia nchi kuongeza pato la taifa.
Ameongeza vita dhidi ya mafisadi inapaswa kuungwa mkono na watanzania wote ili miradi mbalimbali amabyo serikali imepanga kuifanya ifanikiwe kwa wakati.

