
Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa yametajwa kama janga kubwa la kibinadamu kuwahi kutokea nchini humo ndani ya miaka 10 iliyopita. Shirika la kuhudumia watoto UNICEF limesema takribani watoto 16 wameathiriwa na janga hilo.
Kitengo cha maafa nchini Pakistan kinakadiria kwamba katika kipindi cha kuanzia katikati ya mwezi Juni vifo vitokanavyo na mafuriko hayo vimefikia 1,545 ambapo kati ya vifo hivyo 552 ni watoto.
Mamlaka zinasema kwamba huenda idadi ya vifo ikaongezeka kutokana na uwepo wa magonjwa ya homa kali homa ya dengue .