
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Anneth Komba
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TET, Dkt. Anneth Komba, amesema kuwa mabadiliko ya sayansi, teknolojia na uchumi yanapelekea mitaala iliyopo ibadilishwe ili iweze kuendana na mahitaji ya aina ya wahitimu wanaohitajika katika karne hii.
Aidha Dkt. Aneth, amezungumzia utafiti unaofanywa na TET ambao umebaini kuwa watoto wengi hawaelewi wanachofundiahwa, hivyo TET inakuja na tafiti ambayo itawasaidia walimu kufundisha kwa kutumia TEHAMA, jambo litakalosaidia kukuza uelewa kwa wanafunzi.