Jumamosi , 3rd Mar , 2018

Zaidi ya watu 33 wameuwawa katika shambulio jipya lililotokea nchini DRC mauwaji hayo yakihusishwa na fujo za kikabila kati ya jamii ya Hema na Lendu huko kaskazini Mashariki mwa jimbo la Ituri.

Taarifa iliyotolewa na radio ya umoja wa mataifa imesema mapigano hayo yaliweza kudhibitishwa na vyombo vya usalama nchini humo na zaidi ya watu 100 wameuwawa kufuatia vurugu zilizoibuka katika jimbo hilo tangu katikati ya mwezi Desemba mwaka jana.

Mapigana hayo yaliibuka baada ya jamii ya Hema ambayo ni wafugaji na jamii ya Lendi yenye inajihusisha na ukulima katika jimbo hilo la Ituri ambapo jamii hiyo imeendelea kupigana kwa miaka mingi na kusababisha idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani katika kipindi cha miaka miwili.

Inakadiriwa watu 200,000 wamelazimika kuyakimbia makazi yao kufuatia vurugu hizo katika jimbo hilo la Ituri.