Jumanne , 3rd Mei , 2016

Watu laki 4 wanakufa nchini Tanzania kila mwaka kutokana na athali za mabadiliko ya hali hewa ya tabia nchi Tanzania.

Mtaalamu wa masuala ya kinga kutoka Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Azma Simba Kulia na Afisa mfawidhi wa magonjwa Geofrey Mchau Kushoto wakizungumza na vyombo vya habari mapema leo Jijini Dar es salaam

Mtaalamu wa masuala ya kinga kutoka Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Azma Simba amesema watu laki 4 wanakufa nchini Tanzania kila mwaka kutokana na athali za mabadiliko ya hali hewa ya tabia nchi Tanzania.

Dakta Simba ametoa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mabadiliko ya tabia nchi duniani ambayo yanaenda sambamba na mabadiliko ya hali ya hewa na kuongeza kwamba shughuli za kibinadamu zinachangia kwa asilimia 95 kuzalisha na kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha gesi joto kwenye anga hewa na kupelekea baadhi ya watu kupoteza maisha.

Dkt.Simba amesema athali za mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na kuongezeka kwa joto juu ya wastani wakawaida na kuwa na ukame,mafuriko,vimbunga,kubadilika kwa mgawayo na muda wa mvua kunyesha sambamba na kuongezeka kwa kina cha bahari.

Amesema kuwa mabadiliko hayo yameendelea kuleta majanga mbalimbali katika jamii hasa masuala ya kiafya hali inayosababisha ungezeko la magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na yale ya mlipuko na kupeleke ukame uliokithiri.

Ameishauri jamii kuzingatia kanuani za afya wakati wote ili kuepuka magonjwa ya milipuko.