
Basi lililopata ajali
Akithibitisha kutokea kwa ajali hyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara (RPC) George Katabazi amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Septemba 19.2022 ikihusisha basi lenye namba za usajili T 266 APF aina ya mistubish minebas lililokuwa likitokea Matui Wilayani Kiteto kwenda Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.
RPC Katabazi amefafanua kuwa kati ya majeruhi ishirini wa ajali hiyo, majeruhi watatu wamesafirishwa kwenda Dodoma kwa matibabu zaidi.