Jumamosi , 17th Sep , 2022

Watu wawili kati ya 27 waliyojipatia mbolea za ruzuku kwa njia wa udanganyifu na kisha kuziuza kwa wakulima wengine ili kutengeneza faida zaidi,wanashikiliwa na vyombo vya dola wilayani Ludewa mkoani Njombe kwa kuhujumu mfumo upatikanaji wa mbolea uliyowekwa na serikali.

Mbolea ya ruzuku

Mkuu wa Mkoa wa Njombe amelazimika kukutana na maafisa kilimo ,mawakala na makampuni yaliyopewa dhamana ya kutekeleza mpango huo na kisha kupokea ripoti ya mafanikio na changamoto za utekelezaji wake ambapo  badhi ya vionngozi  wanasema hadi sasa wamebaini kuna watu 27 wamepata mbolea kwa njia ya udanganyifu mjini Njombe na kisha kwenda kuziuza tena wilayani Ludewa jambo ambalo ni kinyume cha taratibu.

Baada ya kupokea taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka anatoa onyo kali kwa wakulima, Makampuni na mawakala wanajihusisha na mchezo huo mchafu na kisha kutoa agizo kwa vyombo vya usalama kuingia kazi kuwasaka wahusika wote.

Ili kuboresha mfumo wa upatikanaji wa mbolea za ruzuku kwa wakati,baadhi ya mawakala akiwemo Oraph Mhema na Onesmo Mwajombe wamesema ni vyema serikali ikaongeza idadi ya makampuni yakusambaza mbolea kwani yaliyopo hayaleti mzigo kwa wakati.